Ndugu mdau wa rasilimali za maji,
unakaribishwa sana kwenye tovuti ya ‘Bodi ya Maji ya Bonde la Wami-Ruvu’. Tovuti hii itasaidia wadau kupata uelewa wa Bodi yetu na utendaji kazi wake, kupatiwa huduma zetu, kubadilishana taarifa muhimu, kutoa maoni, kujadili changamoto, kuleta fursa na kupendekeza mbinu bora ya kusonga mbele ili tufikie lengo letu la pamoja la kusimamia Rasilimali za Maji kwa njia endelevu. Ni imani yetu kuwa uwepo wa tovuti hii utaongeza ushiriki wa wadau katika ulinzi na uhifadhi wa vyanzo vya maji kulingana na kauli mbiu yetu ambayo inasema
“Tone la Maji Lazima Lihifadhiwe”




