UTABIRI WA HALI YA WINGI WA MAJI MTO RUVU KWA SIKU 10 ZIJAZO.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeandaa na kuwasilisha utabiri wa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kuzingatia vituo vilivopo katika Kidakio cha Ruvukwa kipindi cha kuanzia tarehe 17 hadi 27 Juni, 2026.
Utabiri huu unalenga kuwezesha wadau wa Mto Ruvu katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi, Viwanda, Utalii na Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira kufahamumwenendo wa wingi wa maji katika mto huo waweze kujua hali ya mwenendo wa wingi wa maji.
Aidha utabiri huu umezingatia utabiri wa hali ya mvua na Jotozilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Utabiri unaonesha kuwa wingi wa maji unaendelea kushuka kutokana na
kupungua kwa Mvua katika safu za Milima ya Uluguru.
Aidha kiwango cha maji kilichopo kwa sasa na utabiri wa siku kumizijazo inaonyesha wingi wa maji uko juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (2009–2024).
Pia kiwango cha maji kilichopo kwa sasa ambayo ni lita 166,000 kwa sekunde pamoja namatarajio ya siku kumi zijazo ni himilivu na kinatosheleza mahitaji ya sektambalimbali, ikiwemo mahitaji ya maji ya majumbaniyanayohudumiwa na mitambo
ya DAWASA ya Ruvu Juu na Ruvu Chini Kwa sasa mahitaji ya maji ni lita 6,000 kwa sekunde.




