1575 – Wami/Ruvu Tuko Site Kikazi Zaidi.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeanza rasmi utekelezaji wa shughuli zake kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ikiwa na dhamira ya kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za maji na kuongeza utoaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo yote ya Bonde la Wami/Ruvu.
Katika mwaka huu wa fedha, Bodi itaendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zinazolenga kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji, kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi na uhifadhi wa rasilimali za maji, kuongeza uelewa kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuhamasisha wananchi kufuata taratibu za kupata vibali vya matumizi ya maji.
Aidha, Bodi itaendelea kuimarisha ukaguzi wa matumizi ya maji ,kufanya tathmini na ufuatiliaji wa vyanzo vya maji, kushirikisha wadau katika uhifadhi wa mazingira yanayozunguka vyanzo vya maji pamoja na kuendesha kampeni za uelimishaji kupitia redio, televisheni na majukwaa mbalimbali ya mawasiliano ili kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi kuhusu usimamizi wa rasilimali za maji.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inatoa wito kwa wananchi na wadau wote kuendelea kushirikiana katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za maji kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
“Tone la Maji Lazima Lihifadhiwe”
#WamiRuvu #1575 #TukoSiteKikaziZaidi#ToneLaMajiLazimaLihifadhiwe#WaterConservationClimateAction




