Wiki ya Utumishi wa Umma 2026.

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma 2026 Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu tumeweka kambi katika Soko la Kingalu lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi wa mazingira.
Elimu hii inalenga kuongeza uelewa wa jamii juu ya wajibu wao katika kulinda Rasilimali za Maji na mazingira kwa maendeleo endelevu.




