Kuelekea Wiki ya Maji 2026.

Kuelekea katika maadhimisho ya Wiki ya Maji 2026, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari ambapo kwa siku ya leo tumepata fursa ya kushiriki moja kwa moja katika kipindi cha Baragumu kinachoruka kupitia Chanel Ten pamoja na Kipindi cha Redio kupitia Magic Fm
Akizungumza katika Kipindi hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Bw. Nickson Lutenda ameeleza mikakati mbalimbali iliyowekwa na Bodi katika uhifadhi wa vyanzo vya maji ili kuwa na uhakika wa huduma ya Majisafi na salama Jijini Dar es salaaam.
Miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na Bodi kuanzisha miradi ya uhifadhi na kuwakwamua wananchi kiuchumi ili waondokane na utegemezi wa moja kwa moja katika mito yetu Hali iliyokuwa ikisababisha uharibifu wa vyanzo vya maji.
Aidha, Bodi inaendelea na zoezi la ufanyaji wa tafiti ya Maji chini Amya ardhi kubaini maeneo kwa ajili ya uchimbaji wa visima hususani katika Jiji la Dar es salaam ili kuboresha Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji.
Bw. Lutenda ametumia wasaa huo pia kutoa wito kwa jamii kuhakikisha wanalinda na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa mustakabali endelevu kwa kizazi cha sasa na cha baadae.
#1575 Tuko Site Kikazi Zaidi.



