DIRA 2050
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Prof. Riziki S. Shemdoe, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, akimwakilisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses M. Kusiluka, akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri pamoja na viongozi wengine, walitembelea banda la Wizara ya Maji na taasisi zake katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma na kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika kulinda na kusimamia vyanzo vya maji.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imehitimisha ushiriki wake katika maonesho hayo kwa kuendelea kuonesha mafanikio mbalimbali katika usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maji pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi endelevu ya maji na utunzaji wa mazingira.
Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, Prof. Shemdoe amemwakilisha Balozi Kusiluka kwa kupongeza juhudi zinazofanywa na Wizara ya Maji pamoja na taasisi zake katika kuimarisha huduma za maji nchini, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza jitihada hizo ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bora, salama na endelevu za maji.
Aidha, ushiriki wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu katika maadhimisho hayo umeendelea kuwa jukwaa muhimu la kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira, utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja na matumizi endelevu ya rasilimali za maji kwa maendeleo ya taifa.

Mpangilio

slot gacor