MARUFUKU SHUGHULI ZA KIBINADAMU NDANI YA HIFADHI YA MAKUTUPORA.

Wataalamu wa WRBWB, Kidakio cha Kinyasungwe kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) wamefanya kikao na wananchi wanaozunguka eneo la hifadhi ya maji chini ya ardhi la Makutupora kwa lengo la kujadili namna bora ya kuishi bila kuharibu mazingira na kuathiri ubora wa maji katika chanzo hicho.
Miongoni mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na usitishwaji wa shughuli zote za kibinadamu ndani ya hifadhi ya maji ikiwa ni pamoja na kilimo, ukataji wa miti, uchomaji wa mkaa na uchungaji wa mifugo katika eneo hilo. Akizungumza katika Kikao hicho, Afisa Kidakio cha maji cha Kinyasungwe Mhandisi Noel Mushi amesisitiza kuwa kwa yeyote atakayekamatwa ameshiriki uharibifu wa mazingira hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
“Tone la maji lazima lihifadhiwe”



