KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2026.

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2026 kimefanyika leo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, yakiwakutanisha viongozi wa serikali, wadau wa mazingira, taasisi mbalimbali na wananchi kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira.
Maadhimisho hayo yamekuwa fursa ya kuonesha mafanikio yaliyopatikana katika kulinda mazingira, kujadili changamoto zinazoendelea kujitokeza pamoja na kuhimiza ushiriki wa kila mwananchi katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa maendeleo endelevu ya Taifa.




