emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

 
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeshiriki katika ziara ya kikazi iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, yenye lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Rais la kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi na salama kuelekea kwa mvua hizo. Ziara hiyo ni sehemu ya hatua za awali za maandalizi ya kukabiliana na maafa yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño zinazotarajiwa na imehusisha taasisi mbalimbali za Serikali zinazoratibu usafi wa mazingira, usimamizi wa mito na masoko.
Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ametembelea Mto Ng’ombe eneo la Tandale na Daraja la Mkwajuni, Wilaya ya Kinondoni pamoja na Mto Msimbazi eneo la Tabata, Wilaya ya Ilala, kwa lengo la kujionea hali ya usafi wa mazingira na kuhakikisha hakuna vizuizi vinavyoweza kuathiri mtiririko wa maji katika maeneo hayo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Chalamila amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wananchi na taasisi za Serikali katika kuchukua tahadhari mapema, hususan kwa kuzuia utupaji wa taka ovyo kwenye mito na mifereji. Ameonya kuwa hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wanaokiuka taratibu za usafi wa mazingira ili kuzuia kuziba kwa njia za maji na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na El-Nino.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kidakio cha Pwani–Wami/Ruvu, Mha. Diana Kimbute, amefafanua changamoto za utupaji taka mitoni na kusisitiza Serikali za Mitaa na Kamati za Mazingira kuhakikisha usafishaji wa mito unafanyika kwa kina, kwa kuondoa tope, taka ngumu na mchanga unaozuia mtiririko wa maji, badala ya kuondoa mchanga pekee. Hatua hiyo itasaidia kuongeza uwezo wa mito kupitisha maji na kupunguza hatari ya mafuriko wakati wa El- nino.

Mpangilio

slot gacor