DC KILAKALA AWATAKA WAMILIKI WA VIWANDA MOROGORO KULINDA AFYA ZA WANANCHI KWA KUDHIBITI MAJITAKA.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amewataka wamiliki wa viwanda mkoani Morogoro kuhakikisha wanalinda afya za wakazi wa mkoa huo kwa kuzingatia ubora wa majitaka yanayotiririka kutoka viwandani pamoja na kurekebisha miundombinu chakavu katika viwanda vyao.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha iliyolenga kujadili usimamizi bora wa majitaka ya viwandani Kilakala amesema lengo la warsha hiyo ni kuimarisha uzingatiaji wa sheria na taratibu za kutibu na kumwaga majitaka katika mito ili kuendelea kulinda ubora wa maji na kuimarisha uwajibikaji kati ya Wami/Ruvu na wamiliki wa viwanda.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Wami/Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuendelea kulinda vyanzo vya maji pamoja na kuhamasisha matumizi ya njia bora na salama za utupaji wa majitaka kwa manufaa ya wananchi na viwanda.
Aidha wadau mbalimbali wameishukuru Wami/Ruvu pamoja na International Union for Conservation of Nature (IUCN) kwa kuandaa warsha hiyo na kutoa elimu sahihi kuhusu njia bora za kutibu majitaka na kuhifadhi mazingira.
"Tonelamajilazimalihifadhiwe"



