NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI ATEMBELEA BANDA LA WAMI/RUVU - DODOMA

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Switbert Zacharia Mkama, leo ametembelea banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu katika Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre Jijini Dodoma.
Dkt. Mkama amepokea taarifa kuhusu majukumu ya Bodi katika usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maji, pamoja na juhudi zinazoendelea kufanyika kulinda vyanzo vya maji na mazingira kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
Katika hatua nyingine Dkt. Mkama ameipongeza Wizara ya Maji kwa juhudi kubwa ya kuwapatika wananchi huduma ya majisafi na salama huku akiitaka Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu kuhakikisha wanaendelea kulinda mazingira kwa kutunza vyanzo vya maji ili visiharibiwe na shughuli za kibinadamu na kusisitiza kuendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowarahisishia wananchi wanaohitaji kuchimbiwa visima.
Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yenye kaulimbiu isemayo “Dira 2050 Tuwajibike Kukijanisha Tanzania,”
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inaendelea kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda lake ili kupata elimu na huduma zinazohusu usimamizi wa rasilimali za maji na mazingira.
“Tone la maji lazima lihifadhiwe “




