DIRA 2050
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Reuben Kwagilwa amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua madhubuti kudhibiti uchimbaji holela wa mchanga na kuimarisha uhifadhi wa mazingira hususan katika vyanzo vya maji na maeneo ya pembezoni mwa mito.
Mhe. Kwagilwa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake katika Mto Msimbazi, iliyolenga kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua pamoja na kubaini changamoto zinazochangia uharibifu wa mazingira.
Amesema shughuli za usafishaji wa mito kupitia uchimbaji wa mchanga zinapaswa kufanyika katika maeneo yaliyoruhusiwa kisheria na kwa kuzingatia masharti ya vibali husika, ili kuepusha athari za mafuriko mmomonyoko wa ardhi na uharibifu wa mazingira.
Aidha amezielekeza mamlaka zinazosimamia mazingira na utoaji wa vibali kufanya ufuatiliaji wa karibu pamoja na tathmini ya mara kwa mara ya vibali vinavyotolewa, ili kuhakikisha masharti ya uhifadhi wa mazingira yanazingatiwa kikamilifu.
Ziara hiyo ilifanyika katika wilaya za Temeke na Kinondoni ikihusisha maeneo mbalimbali ya Mto Msimbazi, kwa lengo la kutathmini changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kuzitatua.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Edward Mpogolo amesema Serikali itaendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria za mazingira, ikiwemo taratibu sahihi za uchimbaji na usafishaji wa mchanga.
Pia amewahimiza wananchi kuepuka kutupa taka kwenye mito na kushiriki katika kulinda vyanzo vya maji, hatua itakayosaidia kupunguza mafuriko na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji kwa jamii.

Mpangilio

slot gacor