DIRA 2050
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

 
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Mathew Kundo (Mb), amepongeza watumishi wa sekta ya maji kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika usimamizi wa rasilimali za maji na utekelezaji wa miradi ya maji nchini.
Mhe. Kundo ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu katika Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika Viwanja vya JK Convention Centre jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kutembelea banda hilo, amesema mchango wa watumishi wa sekta ya maji ni muhimu katika kuhakikisha rasilimali za maji zinalindwa na kutumika kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya taifa.
Aidha, amewataka watumishi hao kuendelea kubuni na kutafuta vyanzo vipya vya maji sambamba na kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa vyanzo vya maji na mazingira ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Mhe. Kundo alisisitiza kuwa mafanikio ya sekta ya maji yanategemea ushirikiano wa karibu kati ya taasisi za serikali, wadau wa maendeleo na wananchi katika kulinda na kuhifadhi rasilimali za maji.
Kwa upande wake, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeendelea kutumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usimamizi endelevu wa rasilimali za maji, uhifadhi wa mazingira na umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji.
Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani mwaka huu yanafanyika chini ya kaulimbiu isemayo, “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania,” ikilenga kuhamasisha jamii kushiriki katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mpangilio

slot gacor