UCHAGUZI WA WAJUMBE WAPYA NA MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO VYAIMARISHA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI MGETA CHINI.

Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wajumbe wapya wa Jumuiya ya Watumia Maji Mgeta Chini (WUA) pamoja na kuanza mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao ili kuboresha usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maji.
Uteuzi wa wajumbe umefanyika kupitia Mabaraza ya Maendeleo ya Kata za Bwakila Chini, Mngazi na Kisaki, zinazojumuisha vijiji vya Bwakila Chini, Mbwade, Bonye, Dakawa, Mngazi, Vigolegole, Sesenga, Milengwelengwe, Gomelo, Kisaki Station, Kisaki Kichangani na Nyarutanga.
Katika mchakato huo Mabaraza ya Maendeleo ya Kata yamezingatia uwakilishi wa makundi mbalimbali ya wadau wa matumizi ya maji ikiwemo vyama vya wakulima, vyama vya wafugaji, skimu za umwagiliaji, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na mazingira, vikundi vya kijamii vinavyohifadhi mazingira, wafyatua matofali, viwanda pamoja na Mamlaka za Maji za Jamii (CBWSO).
Aidha Baada ya uteuzi huo mikutano ya wananchi imefanyika katika vijiji husika kwa lengo la kuthibitisha wajumbe waliopendekezwa, Jumla ya wajumbe 30 wamechaguliwa kutoka vijiji 12 vilivyopo katika kata hizo tatu.
Kutokana na ukubwa wa eneo la Jumuiya ya Watumia Maji Mgeta Chini mipango inaendelea ya kuigawa jumuiya hiyo katika jumuiya mbili ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za maji na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wanachama.
Viongozi na wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wameishukuru Wami/Ruvu kwa kuhuisha jumuiya hiyo wakieleza kuwa hatua hiyo itaimarisha ushiriki wa jamii katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji.
Katika hatua nyingine wajumbe wameanza mafunzo ya kuwajengea uwezo kuhusu usimamizi wa rasilimali za maji, washiriki wamejifunza mada mbalimbali zikiwemo Utambulisho wa Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu, Sera na Sheria za Usimamizi wa Rasilimali za Maji, Majukumu ya Jumuiya za Watumia Maji (WUA)
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuendelea kesho Julai 10, 2026,




