WATAALAMU KUTOKA OFISI YA MKAGUZI MKUU WA NJE WATEMBELEA WAMI/RUVU KUJIFUNZA SHUGHULI ZA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA MAJI.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu leo tarehe 18 juni 2026 imepokea ugeni kutoka Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Nje uliowasili kwa lengo la kujifunza na kupata uelewa kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wami/Ruvu katika usimamizi na uhifadhi wa rasilimali za maji.
Katika ziara hiyo wageni wamepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kimkakati yanayosimamiwa na Wami/Ruvu ili kujionea utekelezaji wa shughuli zake pamoja na mchango wake katika kuhakikisha upatikanaji endelevu wa Rasilimali za Maji kwa wananchi.
Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa ni Bwawa la Mindu lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Bwawa hilo ni chanzo muhimu cha maji kinachohudumia wakazi wa Manispaa ya Morogoro na maeneo ya jirani kwa asilimia 78 hivyo kuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi.




