UTABIRI WA HALI YA WINGI WA MAJI MTO RUVU KWA SIKU 10 ZIJAZO.

Wami/Ruvu imeandaa na kuwasilisha utabiri wa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kuzingatia vituo vilivopo katika Kidakio kwa kipindi cha kuanzia tarehe 29 Mei hadi 07 Juni, 2026.
Utabiri huu unalenga kuwezesha wadau wa Mto Ruvu katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi, Viwanda, Utalii na Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira kufahamu mwenendo wa wingi wa maji katika Mto Ruvu waweze kujua hali ya mwenendo wa wingi wa maji.
Aidha utabiri huu umezingatia utabiri wa hali ya mvua na Jotozilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Utabiri unaonesha kuwa wingi wa maji utaendelea juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (2009–2024)kuanzia tarehe 04 Juni,2026 kutokana na Mvua kidogo inayotarajiwa kunyesha katika safu za Milima ya Uluguru mwanzoni mwa Mwezi Juni.
Aidha kiwango cha maji kilichopo kwa sasa ambayo ni lita 57,000 kwa sekunde pamoja na matarajio ya siku kumi zijazo ni himilivu na kinatosheleza mahitaji ya sekta mbalimbali ikiwemo mahitaji ya maji ya majumbani yanayohudumiwa na mitambo ya DAWASA ya Ruvu Juu na Ruvu Chini.
"Tonelamajilazimalihifadhiwe"



