DIRA 2050
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

 
Kikao hicho kilijikita katika kupitia mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza ufanisi katika usimamizi na maendeleo ya Rasilimali za Maji ndani ya Bonde la Wami/Ruvu.
 
Katika majadiliano hayo wajumbe wamepokea na kuchambua Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli zilizopangwa kwa kipindi cha Robo ya Pili zikiwemo shughuli za uhifadhi wa vyanzo vya maji, usimamizi wa matumizi endelevu ya maji, utoaji wa elimu kwa jamii pamoja na hatua zinazochukuliwa kudhibiti uharibifu wa mazingira unaoweza kuathiri upatikanaji wa maji.
 
Aidha wajumbe wamesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi za Serikali, wadau wa maendeleo na jamii katika kuhakikisha Rasilimali za Maji zinatunzwa na kutumika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi Nickson Lutenda ameeleza kuwa utekelezaji wa Mpango Kazi unaendelea vizuri licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali huku akitoa rai kwa watendaji kuongeza uwajibikaji na kasi ya utekelezaji wa shughuli zilizobaki katika mwaka wa fedha 2025/2026.
 
Kikao hicho ni sehemu ya jitihada za Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu kuhakikisha usimamizi bora wa Rasilimali za Maji, kuimarisha huduma kwa wananchi pamoja na kuchochea maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
 
 
"Tonelamajilazimalihifadhiwe"

Mpangilio

slot gacor