Kidakio cha Ngerengere wafanya usafi Mto Morogoro.

Katika kuadhimisha Siku ya Kilele cha Mazingira Duniani Kidakio cha Ngerengere pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira wamefanya shughuli ya usafi katika Mto Morogoro eneo la Daraja la Kichangani mkoani Morogoro.
Mbali na kufanya usafi wa mazingira pia imetolewa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira kudhibiti utupaji holela wa taka na kulinda vyanzo vya maji ili kuhakikisha mazingira yanabaki safi na salama kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Katika kuendeleza juhudi hizo wametembelea na kugawa vifaa vya usafi katika shule za msingi za Msufini, Mwere na Chamwino ambapo pia wamezungumza na wanafunzi na walimu kuhusu umuhimu wa usafi wa mazingira shuleni na katika jamii kwa ujumla.
Shughuli hiyo ni sehemu ya jitihada za kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa maendeleo endelevu.




