emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Mhandisi Mwajuma Waziri, Katibu Mkuu Wizara ya Maji amezindua Warsha ya kujengewa uwezo kwa Timu za Utekelezaji wa Mradi wa Bonde la Mkondoa chini ya WRBWB wenye thamani ya kiasi cha Shilingi Bilioni 14 na Mradi wa Uboreshaji huduma ya maji na usafi wa mazingira katika vijiji 24 vya Ngerengere chini ya RUWASA wenye thamani ya Shilingi Bilioni 22. 

Wakati akifungua Warsha hiyo amebainisha kuwa Miradi hii inaendana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 inayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi sambamba na kuendana na mipango ya ndani ya kuhakikisha kuwa vijiji 1575 visivyo na huduma ya maji nchini vinafikiwa. 

Kwa upande wake Robert Sunday, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji wa Wizara ya Maji ametanabaisha kuwa Wizara kupitia Kurugenzi ya Rasilimali za Maji itatoa usimamizi wa kisheria, mwongozo wa kiufundi, na msaada wa kujenga uwezo kwa Wataalam na amesisitiza kuwa mafanikio ya utekelezaji wa miradi hiyo yanategemea ushirikiano, uwajibikaji, na ushiriki wa jamii nufaika.

Katika hatua nyingine Mhandisi Elibariki Mmasy Mkurugenzi wa WRBWB ameeleza kuwa Bonde la Mkondoa ni muhimu kwa maisha, kilimo, na mifumo ya ikolojia kwa idadi kubwa ya watu akithibitisha kuwa eneo hilo linakabiliwa na mafuriko, ukame wa muda mrefu, na uharibifu wa ardhi. 

Ametoa wito kwa wadau wote kushiriki kikamilifu katika utekelezaji na kulinda uwekezaji huo kwa vizazi vya sasa na baadae.

Aidha Wataalam wa Wizara ya Maji wametoa Shukrani kwa Maandalizi ya maandiko ya miradi kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kuonesha nia ya kufadhili miradi hiyo kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwataka Timu za Uratibu wa Utekelezaji wa miradi hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni wakati wa utekelezaji.

#Tonelamajilazimalihifadhiwe

Mpangilio