RC SENDIGA AIPONGEZA WAMI/RUVU KWA JITIHADA ZA KUKABILIANA NA MAFURIKO.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Queen Sendiga kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama ya Wilaya amefanya ziara ya kukagua maeneo yanayokabiliwa na hatari ya mafuriko wakati wa msimu wa mvua.
Maeneo yaliyotembelewa ni pamoja na Kihonda, Azimio, Lukobe, Kwa Bwana Jela na Korongo la Tushikamane katika Manispaa ya Morogoro.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameipongeza Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa juhudi za kurejesha mito iliyopoteza mwelekeo wake katika njia zake za asili ikiwemo Mto Ngerengere hatua inayolenga kupunguza athari za mafuriko.
Aidha amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuepuka kutupa taka hovyo zinazoweza kuziba njia za maji pamoja na kuwaasa wanaoishi pembezoni mwa mito kuhamia maeneo salama ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa.
Tonelamajilazimalihifadhiwe



