emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

 
Wananchi wa Kata ya Kikongo, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, wamepatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi Bwawa la Kiembaemba lililopo Kitongoji cha Mwanabito, ili kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika kwa uendelevu bila kuathiri mazingira.
Mafunzo hayo yametolewa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Mfuko wa Uhifadhi wa Mazingira Duniani (WWF), yakihusisha wakulima, wafugaji na wavuvi wanaotegemea bwawa hilo katika shughuli zao za kiuchumi, zikiwemo kilimo cha umwagiliaji, ufugaji na uvuvi.
Kupitia mafunzo hayo, wananchi wamejengewa uelewa kuhusu matumizi sahihi ya maji na kuepuka vitendo vinavyoweza kusababisha uchafuzi na uharibifu wa bwawa hilo, huku wakieleza kuwa elimu hiyo itawasaidia kulitunza kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima, Bi. Sophia Hassan amesema mafunzo hayo yatawawezesha kuendeleza kilimo cha umwagiliaji kwa kuzingatia taratibu bora za matumizi ya maji na utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake, Bw. Charles Masoya, mfugaji, amesema elimu hiyo imewasaidia kuelewa namna bora ya kuwapatia mifugo maji bila kuwaingiza ndani ya bwawa, ili kuzuia uchafuzi na uharibifu wa chanzo hicho.
Naye Afisa Mazingira wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Bi. Bibiana Abeli, amesema mafunzo hayo yamefanikiwa na wananchi wa makundi yote matatu wameonesha uelewa kuhusu umuhimu wa kutumia na kuhifadhi bwawa hilo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeendelea kushirikiana na wananchi kutoa elimu kuhusu uhifadhi wa rasilimali za maji, ikiwemo mito, mabonde na mabwawa, ili kuhakikisha zinatumika kwa uendelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Mpangilio

slot gacor