KAMATI YA KIDAKIO CHA RUVU YAPITIA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI NA KUWEKA MIKAKATI YA 2026/2027

Kamati ya Kidakio cha Ruvu ikiongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Praxeda Kalugendo imefanya kikao chake cha kawaida kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa shughuli mbalimbali na kuweka mikakati ya kuboresha utendaji kwa mwaka wa fedha ujao.
Katika kikao hicho wajumbe wamepitia taarifa ya utekelezaji wa kazi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo wamejadili mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizojitokeza katika kipindi kinachohitimishwa mwezi Juni 2026.
Wajumbe wametoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kutatua changamoto hizo na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Kidakio cha Ruvu.
Aidha kikao hicho kimejadili na kupitia rasimu ya mpango kazi wa mwaka wa fedha 2026/2027, huku wajumbe wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano, uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa shughuli za maendeleo ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa kwa ufanisi.
Kamati imehitimisha kikao kwa kuazimia kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kutekeleza majukumu yake na kuhakikisha maamuzi yaliyofikiwa yanatekelezwa kwa wakati kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya eneo la Kidakio cha Ruvu.
"Tonelamajilazimalihifadhiwe"




