HOTUBA YA WAZIRI WA MAJI BUNGENI DODOMA KIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAJI.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema kuwa hadi kufikia mwezi Aprili, 2026 shughuli za usimamizi wa rasilimali za maji zimehusisha kujenga na kukarabati vituo 256 vya kufuatilia mwenendo wa rasilimali za maji, kutoa vibali 306 vya matumizi ya maji, vibali 40 vya ujenzi wa mabwawa ya topesumu, vibali vitatu (3) vya ujenzi wa mabwawa ya maji, vibali 1,177 vya kuchimba visima, vibali 247 vya kutiririsha majitaka, leseni 24 za utafiti, leseni 120 za wachimbaji na leseni 62 za kampuni za uchimbaji visima, kutatua migogoro 15 ya matumizi ya maji, kusajili mabwawa nane (ya topesumu; kusajili mabwawa 6, kupanda miti zaidi ya milioni 6 kwenye vyanzo vya maji, kujenga mabirika 55 ya kunyweshea mifugo, pamoja na kuweka mipaka katika vyanzo vya maji 359.




