UTABIRI WA HALI YA WINGI WA MAJI MTO RUVU - 05 Okt. 2026

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeandaa na kuwasilisha utabiri wa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kuzingatia vituo vilivopo katika vidakio kwa kipindi cha kuanzia tarehe 5 Oktoba hadi 15 Oktoba, 2026.
Utabiri huu unalenga kuwezesha wadau wa Mto Ruvu katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi, Viwanda, Utalii na Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira kufahamu mwenendo wa wingi wa maji katika mto huo ili waweze kujua hali ya mwenendo wa wingi wa maji.
Aidha, utabiri huu umezingatia utabiri wa hali ya mvua na Joto zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
Utabiri unaonesha kuwa wingi wa maji umeendelea kupungua kutokana na uhaba wa mvua katika safu za Milima ya Uluguru ambayo ndiyo chanzo cha Mto Ruvu.
Aidha, kiasi cha maji kilichopo kwa sasa kiko chini ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (2009–2024).
Pia, kiwango cha maji kilichopo kwa sasa ambayo ni lita 9,700 kwa sekunde pamoja na matarajio ya siku kumi zijazo ni himilivu na kinatosheleza mahitaji ya sekta mbalimbali, ikiwemo mahitaji ya maji ya majumbani yanayohudumiwa na mitambo ya DAWASA ya Ruvu Juu na Ruvu Chini. Kwa sasa, mahitaji ya maji ni lita 6,000 kwa sekunde.
Bodi itaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa wingi wa maji kila baada ya siku kumi na kuwahabarisha watumiaji na Mto Ruvu ili waendelea kuchukua hatau za tahadhari dhidi ya kuongezeka/kupungua kwa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa siku zijazo.



