Utabiri wa Hali ya Wingi wa Maji katika Mto Ruvu - 12-22 Machi 2026.

WRBWB imeandaa na kuwasilisha utabiri wa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kuzingatia vituo vilivopo katika idakio kwa kipindi cha kuanzia tarehe 12 hadi 22 Machi 2026 ambapo utabiri huu unalenga kuwezesha wadau wa Mto Ruvu katika sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi, Viwanda, Utalii na Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira kufahamu mwenendo wa wingi wa maji katika mto huo.
Utabiri huu umezingatia hali ya mvua na joto kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambapo unaonesha kuwa wingi wa maji utakuwa juu ya wastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (2009–2024). Hali hii inachangiwa na uwepo wa mvua zinazoendelea kunyesha katika safu ya Milima ya Uluguru.
Aidha, kiwango cha maji kilichopo kwa sasa pamoja na matarajio ya siku kumi zijazo ni himilivu na kinatosheleza mahitaji ya sekta mbalimbali, ikiwemo mahitaji ya maji ya majumbani yanayo hudumiwa na mitambo ya DAWASA ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ambapo Kwa sasa, mahitaji ya maji ni mita za ujazo sita (6) kwa sekunde.
Bodi inapenda kuwashauri watumiaji wa Maji katika sekta tajwa kuchukua tahadhari dhidi ya ongezeko la maji katika Mto Ruvu hali inayowezapelekea upotevu wa mali, uharibifu wa miundombinu na athari nyingine za kiuchumi na kijamii.
Bodi itaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa wingi wa maji kila baada ya siku kumi na kuwahabarisha watumiaji na Mto Ruvu ili waendelea kuchukua hatau za tahadhari dhidi ya kuongezeka/kupungua kwa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa siku zijazo.
#1575 Tuko Site Kikazi Zaidi



