UTABIRI WA HALI YA WINGI WA MAJI MTO RUVU MWEZI JUNI HADI AGOSTI 2026.

Wami/Ruvu imeandaa na kuwasilisha utabiri wa hali ya wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kipindi cha Mwezi Juni hadi Agosti, 2026 ili wadau wa Mto Ruvu katika sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ujenzi, Viwanda, Utalii na Mamlaka za Maji Safi na Usafi wa Mazingira waweze kujua hali ya mwenendo wa wingi wa maji.
Aidha utabiri huu umezingatia utabiri wa hali ya mvua na Joto kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kipindi cha Mwezi Juni hadi Agosti, 2026.
Utabiri unaonyesha mwelekeo wa wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kipindi cha Mwezi Juni – Agosti, 2026 utakuwa Juu yaWastani ukilinganisha na wastani wa muda mrefu (2009 – 2024) pamoja na utabiri wa Mwaka 2025 kama inavyoonekana katika Kielelezo, hii ni kutokana na utabiri wa hali ya mvua kutoka TMA ambao unaonyesha kutakuwa na mvua zitakazo endelea kunyesha hadi Mwezi Agosti, 2026 katika maeneo ya Kidakio cha Mto Ruvu.
Aidha Utabiri unaoyesha kiasi cha maji kilichopo kwa sasa na baada ya miezi mitatu (Juni -Agosti 2026) kitatosheleza mahitaji ya Sekta tajwa hapo juu ambayo ni mita za ujazo sita (6) kwa sekunde.
Utabiri unaonyesha kwa Kipindi cha Mwezi Juni -Agosti, 2026 wastani wa ujazo wa maji utafikia mita za ujazo milioni 468.3. Ujazo huu ungeweza kujazaBwawa la Kidunda yenye uwezo wa mita za ujazo Milioni 190 kwa asilimia 100 kama Ujenzi wa Bwawa ungekuwa umekamilika.
Bodi itaendelea kufuatilia kwa ukaribu zaidi hali ya wingi wa maji katika Mto Ruvu kwa kufanya utabiri wa vipindi vifupi vya kila baada ya siku kumi na kuwahabarisha wadau wake ili waendelea kuchukua hatau za tahadhari dhidi ya kuongezeka/kupungua wingi wa maji utakaoweza kujitokeza.




