WANAFUNZI WAIPONGEZA WAMI/RUVU KWA JUHUDI KUBWA ZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana, IUCN Tanzania na Manispaa ya Morogoro wameendelea kutekeleza zoezi la ugawaji wa miti ya matunda kwa wakazi wa Kata ya Mzinga Manispaa ya Morogoro.
Zoezi hilo pia limehusisha Taasisi za Elimu ikiwemo Shule ya Sekondari Konga na Shule ya Msingi Konga ambapo wanafunzi na walimu wamepatiwa miche hiyo kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa mazingira tangu ngazi ya shule.
Ugawaji huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji unaolenga kupunguza athari za uharibifu wa mazingira, kuongeza uoto wa asili pamoja na kuboresha maisha ya jamii kupitia upatikanaji wa matunda na kivuli.
Wananchi wa Kata ya Mzinga wamehimizwa kuitunza na kuikuza miti hiyo ili kufanikisha malengo ya mradi huo huku wadau wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii katika kulinda mazingira kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.
"Tonelamajilazimalihifadhiwe"



