Taarifa ya utabiri wa mafuriko kuanzia tarehe 28 Machi hadi 06 Aprili 2026.

Taarifa ya utabiri wa mafuriko inaonesha Kuna uwezekano wa ongezeko la wastani na Juu ya wastani la wingi wa maji katika baadhi ya mito ambalo linaweza kupelekea mafuriko katika kipindi cha kuanzia tarehe 28 Machi hadi 06 Aprili 2026.
Aidha Kwa mujibu wa utabiri umebainisha baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kukumbwa na mafuriko ambay hi Kijji cha Ving’awe, Zombo Tindiga, Daraja la Mkundi, Mkata,Miyombo, Munisigara, Masanze, Kibaoni, Malui, Magomeni-Kilosa, Gulwe, Kilimanjaro, Kisala, Berega Darajani na Changalawe Kilosa.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inatoa wito kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kuchukua tahadhari ili kujilinda na athari zinazoweza kujitokeza huku Mamlaka husika zinasisitizwa kuondoa vizuizi vya maji katika madaraja ili kuruhusu mtiririko sahihi wa maji na kupunguza hatari ya mafuriko.
Bodi itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa viwango vya mitiririko ya maji na kutoa taarifa zaidi
“Tone la maji lazima lihifadhiwe “



