Wizara ya Maji Wakagua Chanzo cha Maji Makutupora

Wizara ya Maji imekagua chanzo cha maji cha Makutupora ambacho kinategemewa katika jiji la Dodoma
Ukaguzi umeongozwa na watalaamu wa Idara ya Rasilimali za Maji kwa kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu pamoja na Bodi ya Maji Bonde la Kati, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji nchini.
Lengo mahsusi limekuwa kuongeza ufanisi katika uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za maji, na kutumia kama jukwaa la mafunzo kwa watumishi.
Ukaguzi umewezesha, watumishi kupata fursa ya kujifunza kwa vitendo kuhusu usimamizi wa maji chini ya ardhi, mbinu za ufuatiliaji wa vyanzo vya maji pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Chanzo cha maji cha Makutupora bado kinaendelea kuwa tegemeo kuu la upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Jiji la Dodoma,
Ni rasilimali nyeti inayohitaji uangalizi na usimamizi wa karibu zaidi. Kutokana na umuhimu huo, ziara hiyo imebainisha haja ya kuimarisha tathmini za rasilimali za maji, kuongeza matumizi ya tafiti za kisayansi pamoja na kuendeleza mifumo madhubuti ya kufuatilia hali ya maji chini ya ardhi.
“Dodoma ni Makutupora na Makutupora ni Dodoma”
1 5 7 5: Maji, Tuko Site, Kikazi Zaidi




