Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Morogoro imefanya ziara maalumu ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Sekta ya Ma

Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Morogoro imefanya ziara maalumu ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Sekta ya Maji ambapo wamekagua vyanzo vya maji na miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa maji Mkoani Morogoro.
Akizungumza Katika Ziara hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Bw. Joseph Masunga ameridhishwa na hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama huku akisisitiza suala la utunzaji wa vyanzo vya maji lipewe kipaumbele ili kuwa na uhakika wa huduma ya maji endelevu.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa WRBWB Mhandisi Elibariki Mmassy amebainisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuimarisha utunzaji wa rasilimali za maji ikiwa ni pamoja na upandaji wa miti, utoaji wa elimu wa jamii pamoja na kuwapatia shughuli mbadala wananchi ili waishi rafiki na mazingira.



