Makamu wa Rais azindua Mfumo wa Kutabiri Kiasi cha Maji kwenye Mito.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Emmanuel Nchimbi amezindua Mfumo wa Utabiri wa Kiasi cha Maji kwenye mito nchini Tanzania.
Uzinduzi huo umefanyika katika la Bwawa la Mindu Mjini Morogoro ambako amejionea namna Wizara ya Maji inavyoshiriki katika utunzaji, ulinzi na Uendelezaji wa Rasilimali za Maji.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Mkurugenzi wa Bodi, Mhandisi Elibariki Mmassy amesema mfumo huo ni Moja ya jitihada za Wizara ya Maji kuhakikishia inaondoa changamoto za Sekta kwa kuwezesha upatikanani wa taarifa sahihi za kiwango cha Maji.
Amesema Bwawa Hilo ni sehemu ya maeneo yatakayonufaika na changamoto hiyo kwani linapokea maji kutoka sehemu mbalimbali za nchi na linachangia kwa zaidi ya asilimia 70 ya huduma ya Majisafi katika mji wa Morogoro.



