emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 umezindua Mradi wa uhifadhi wa chanzo cha Ruvu kupitia Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji Maji katika Vijiji vya Mngazi na Dakawa, uliotekelezwa na kusimamiwa na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa lengo la kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuwapatia wananchi huduma bora ya maji safi na salama vijijini.
Mradi huu umehusisha uchimbaji wa visima viwili vyenye uwezo wa kuzalisha maji kati ya lita 248,000 kwa saa , ujenzi wa mtandao wa bomba wenye jumla ya kilomita 26, Vituo vya kuchotea maji 34, ujenzi wa pump house na uwekaji wa pump za kusukuma maji zenye uwezo wa kati ya lita 30,000 kwa saa Mngazi hadi lita 50,000 kwa saa Dakawa pamoja na ujenzi wa matenki 2 yenye ujazo wa lita 160,000
Mbali na kuboresha upatikanaji wa maji, mradi huu umejenga birika la kunyweshea mifugo katika Kitongoji cha Lukenze, Kijiji cha Dakawa, hatua inayosaidia kupunguza migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Mradi umegharimu shilingi bilioni 3.18 ambapo kwa sasa unawanufaisha wakazi Elfu 6,453 wa vijiji vya Mngazi na Dakawa, huku idadi hiyo ikitarajiwa kufikia watu 11,550 ifikapo mwaka 2043
Akizungumza katika Hafla hiyo ya uzinduzi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 Ndugu Wazo Michael Mwang’onda amebainisha kuridhishwa na ubora wa mradi huu na kuwataka wananchi kutunza na kulinda rasilimali za maji ili kuwa na uhakika wa huduma za majisafi na salama.

Mpangilio

slot gacor