Wami/Ruvu imefanikiwa kukamilisha uchimbaji wa kisima cha maji chenye zaidi ya mita 30 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imefanikiwa kukamilisha uchimbaji wa kisima cha maji chenye zaidi ya mita 30 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, hatua inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa maji ya uhakika.
Kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita za ujazo elfu 20 kwa saa, kiwango ambacho kinatajwa kuwa cha kutosha kuhudumia mahitaji ya maji katika ofisi zote za wizara hiyo pamoja na taasisi na wananchi wanaozunguka eneo hilo.
Mradi huo umetajwa kuwa chanzo muhimu cha maji mbadala kitakachosaidia kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji wakati wa dharura au upungufu wa huduma kutoka vyanzo vingine.
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inaendelea na uchimbaji wa visima vya maji katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam ili kuongeza huduma ya upatikanaji wa majisafi na salama.



