WAMI/RUVU YAANZA UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI IGUNGILO

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Wizara ya Maji imebaini maeneo mawili yenye viashiria vya uwepo wa maji chini ya ardhi katika Kijiji cha Igungilo, Wilaya ya Chamwino,, Dodoma baada ya kufanya utafiti wa kijiofizikia kwa ajili ya kuandaa hatua za uchimbaji wa kisima.
Utafiti huo umefanyika kwa kutumia Magnetic Survey na Vertical Electrical Sounding (VES), ambapo data zilizokusanywa zinaendelea kufanyiwa uchambuzi wa kitaalamu ili kubaini eneo lenye uwezekano mkubwa zaidi wa maji na kina kinachofaa kwa uchimbaji.
Zoezi hilo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa 1-5-7-5 wa kuharakisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi. Bodi inaendelea na utafiti katika maeneo mengine, huku ikisisitiza kuwa uwepo wa maji utathibitishwa baada ya hatua za uchimbaji na vipimo vya kisima kukamilika.



