WAMI/RUVU YAPONGEZWA KWA JUHUDI ZA UHIFADHI WA VYANZO NA MAZINGIRA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni amesema Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira hauwezi kufanikiwa kwa kauli au sera peke yake, bali kwa vitendo vinavyoonekana katika ngazi zote ikiwemo shughuli za kupanda miti na kuitunza.
Amesema Dira ya Taifa ya mwaka 2050 ina nguzo kuu tatu na miongoni mwa nguzo hizo ni suala zima la uhifadhi wa mazingira na ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi jambo ambalo kila mmoja anapaswa kulitazama kwa upana wake na kupongeza juhudi za maksudi zinazofanywa Bodi ya maji Bonde la Wami/Ruvu katika upandaji miti na utunzaji wa Vyanzo na Mazingira kwa Ujumla.
Waziri Masauni ameyasema hayo Mei 15, 2026 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kwenye zoezi la upandaji miti ili kuhakikisha Mazingira yanabaki kuwa salama kutokana na uoto wa asili ikiwa ni shughuli zinazopangwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani itakayofanyika Juni 5 mwaka huu ambapo kitaifa itafanyika mkoani Dodoma.
"Tone la maji lazima lihifadhiwe"




