DIRA 2050
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

 
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imekamilisha uchimbaji wa kisima chenye kina cha zaidi ya mita 120 katika eneo la Kijichi Mtoni, jijini Dar es Salaam, hatua inayotarajiwa kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Kata ya Kijichi na maeneo ya jirani.
Kwa sasa kisima hicho kinaendelea na hatua ya usafishaji wa kisima (flushing), ambayo ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kutumika rasmi. Zoezi hilo linafanyika ili kuondoa chembechembe zilizobaki baada ya uchimbaji na kuhakikisha maji yanayozalishwa ni safi, salama na yanakidhi viwango vya ubora kwa matumizi ya binadamu.
Utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya juhudi za Serikali kupitia Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu za kuimarisha upatikanaji wa maji kwa kutumia vyanzo mbadala vya maji chini ya ardhi. Hatua hiyo inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji na kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutokana na ukuaji wa idadi ya watu.
Wananchi wa Kata ya Kijichi pamoja na maeneo ya jirani wanatarajiwa kunufaika na mradi huo kupitia upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika, hatua itakayopunguza adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji na kuboresha ustawi wa jamii pamoja na shughuli za kijamii na kiuchumi.
Wami/Ruvu itaendelea kutekeleza miradi ya uchimbaji wa visima katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kuzingatia tathmini za kitaalamu za rasilimali za maji chini ya ardhi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama kwa uhakika, sambamba na kuimarisha usimamizi endelevu wa rasilimali za maji.

Mpangilio

slot gacor