emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Wataalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu wamefanya tathmini ya kitaalamu katika visima vitatu vya maji vilivyopo ndani ya eneo la Bunge la Tanzania, jijini Dodoma, kwa lengo la kubaini hali ya visima na kuhakikisha vinaendelea kutoa huduma kwa ufanisi na usalama.
Katika zoezi hilo, wataalamu hao walipima kina cha maji (water depth) katika visima hivyo vitatu ili kufahamu kiwango cha maji kilichopo, walifanya uchunguzi wa ubora wa maji (water quality) ili kubaini kama yanakidhi viwango vinavyotakiwa kwa matumizi husika, pamoja na kukagua miundombinu ya visima ili kutathmini hali yake ya kiutendaji.
Aidha, walitekeleza Pumping Test katika visima hivyo vitatu, kipimo cha kitaalamu kinachotumika kubaini uwezo wa kisima kuzalisha maji, kiwango kinachoweza kuvunwa kwa usalama na mwenendo wa urejeaji wa maji ndani ya tabaka la maji ardhini. Matokeo ya vipimo hivyo husaidia katika kufanya maamuzi sahihi kuhusu matumizi endelevu ya visima na upangaji wa matengenezo ya miundombinu ya maji.
Zoezi hilo linaakisi jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Maji za kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji na kuhakikisha taasisi zote muhimu zinaendelea kupata huduma bora za maji kwa maendeleo ya Taifa.
Zoezi hilo ni sehemu ya majukumu ya Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu katika kusimamia, kulinda na kuendeleza rasilimali za maji nchini, sambamba na kuhakikisha miundombinu ya maji inayohudumia taasisi muhimu za Taifa inaendelea kuwa salama, imara na endelevu.

Mpangilio

slot gacor