WAMI/RUVU YAENDELEA NA ZOEZI LA UCHIMBAJI VISIMA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM NA PWANI

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu inaendelea na zoezi la uchimbaji wa visima vya maji kwenye maeneo yote yenye changamoto ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama hususani katika Jiji la Dar es salaam na Pwani ambapo kwa siku ya Leo limefanyika zoezi la ukaguzi wa kazi inayoendelea katika Mtaa wa Viziwaziwa, Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
Uchimbaji huu unafanyika na mitambo inayomilikiwa na Bodi ambapo mpaka sasa maeneo 19 tayari yameshafanyiwa tafiti ya maji chini ya ardhi na uchimbaji umeanza rasmi chini ya usimamizi kutoka kwa wataalam wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu.
“Tone la maji lazima lihifadhiwe “



