emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Bodi ya Maji ya Bonde la Wami/Ruvu imeendesha mafunzo maalum ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora (Quality Management System – QMS) yenye lengo la kuimarisha uwezo wa watumishi na kuwaandaa Wakaguzi wa Ndani kuelekea kupata ithibati (accreditation) ya kimataifa.
Mafunzo hayo yamehusisha nadharia na ukaguzi kwa vitendo (practical auditing) ambapo washiriki wamepata fursa ya kufanya tathmini ya mifumo na taratibu za utendaji kazi ndani ya taasisi.
Kupitia zoezi hilo changamoto mbalimbali za kiutendaji zimebainishwa na kutolewa mapendekezo ya maboresho yanayopaswa kufanyiwa kazi kwa wakati ili kujenga mfumo imara wa utendaji wenye uwajibikaji, ufanisi na kuzingatia viwango vya ubora vinavyotambulika kimataifa.
Hatua hii ni sehemu ya juhudi za Bodi katika kuendelea kuimarisha mifumo yake ya usimamizi wa ubora, sambamba na kuhakikisha kuwa huduma na bidhaa za kihaidrolojia zinazozalishwa zinakidhi viwango vya juu vya kitaaluma na mahitaji ya wadau mbalimbali.
Aidha Kupata ithibati ya kimataifa kutachangia kuongeza usahihi, usalama na uaminifu wa data za kihaidrolojia zinazotolewa kwa wadau, watunga sera na wawekezaji wa kimkakati, hatua hiyo itasaidia kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema dhidi ya majanga ya mafuriko na ukame kwa kuhakikisha taarifa zinazotolewa zinakuwa sahihi za wakati na zenye kuaminika.
Vilevile utekelezaji madhubuti wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora utawezesha utoaji wa huduma za Rasilimali za maji ndani ya Bonde la Wami/Ruvu kuendana na viwango vya kisasa, endelevu na vyenye tija ya muda mrefu na kuchangia maendeleo ya sekta ya maji na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Wami/Ruvu inaendelea kujizatiti katika kuboresha mifumo yake ya utendaji ili kuhakikisha huduma bora, uwajibikaji mkubwa na matumizi sahihi ya taarifa za Rasilimali za Maji kwa maendeleo endelevu ya nchi.

Mpangilio

slot gacor