WAMI/RUVU YASAMBAZA DAWA ZA KUDHIBITI WADUDU KATIKA MAENEO YALIYOPANDWA MITI.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (IUCN), imesambaza dawa za kudhibiti wadudu katika maeneo yaliyopandwa miti kwa lengo la kuhakikisha miti hiyo inakua vizuri na kuendelea kustawi.
Miongoni mwa maeneo yaliyopokea dawa hizo ni Gwata, Shule ya Sekondari Kongo pamoja na Shule ya Safina katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Dawa hizo zinatarajiwa kusaidia kudhibiti na kuua wadudu hatarishi wanaoshambulia miti ambao huathiri ukuaji wa miti na wakati mwingine kusababisha baadhi ya miti kukauka na kufa.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na wadau katika kuhakikisha maeneo yaliyopandwa miti yanalindwa na miti hiyo inakua kwa afya hivyo kuchangia katika uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji.
Tonelamajilazimalihifadhiwe



