Wami/Ruvu yatoa reflector 40 kwa Boda boda.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imetoa reflector 40 kwa dereva usafirishaji (Boda boda) katika Soko la Chifu Kingalu, Morogoro, ikiwa ni sehemu ya kuthamini mchango wao kama mabalozi wa utunzaji wa rasilimali za maji.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Wiki ya Huduma kwa Wateja, ambapo Bodi ya WAMI/RUVU imeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza na kulinda rasilimali za maji.
Katika kampeni hiyo, Bodi imewafikia pia maafisa usafirishaji boda boda kwa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa kutovipeleka vyombo vyao vya moto katika mazingira ya vyanzo vya maji kwa ajili ya kuviosha, hatua ambayo inaweza kuchangia uchafuzi wa vyanzo hivyo.
Mwenyekiti wa Soko la Chifu Kingalu, Khalid Mkunyagela, amepongeza jitihada zinazofanywa na Wami/Ruvu katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu utunzaji wa rasilimali za maji.
Mkunyagela amesisitiza pia umuhimu wa maafisa usafirishaji kushirikiana katika kulinda mazingira kwa kutoshiriki kusafirisha takataka ambazo hutupwa katika maeneo ya vyanzo vya maji.



