WAMI/RUVU YATUNUKIWA TUZO MBILI ZA UTENDAJI KAZI BORA MIONGONI MWA MABONDE 9 YA MAJI NCHINI.

WRBWB imeibuka kinara kwa kushika namba moja na kupokea tuzo 2 za Utendaji Bora wa Kazi (Best Performing Basin Water Board) pamoja na Tuzo ya Utoaji wa taarifa kuhusu tabiri za mafuriko (Best Perfoming in Flood Forecating) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango unaofanywa na Wami/Ruvu katika usimamizi wa Rasilimali za maji miongoni mwa Bodi za maji za mabonde 9 Zilizopo nchini.
Tuzo hizo zimekabidhiwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso, leo Januari 28, 2026 wakati akifungua Mkutano wa Mwaka wa Tisa wa Bodi za Maji za Mabonde Mkoani Dodoma ambapo ameipongeza Wami/Ruvu kwa kuendelea kuwa Bonde la mfano katika utekalazaji wa majukumu yake.
Tuzo hizi zinaonesha dhamira ya Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu katika kusimamia Rasilimali za Maji kwa weledi, matumizi ya Sayansi na Teknolojia, pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha maji yanapatikana kwa uhakika na kwa uendelevu.



