WAMI/RUVU WAFANYA KIKAO CHA KWANZA CHA BAJETI YA BODI YA SABA.

WRBWB imefanya kikao chake cha Kwanza cha Bajeti ya Bodi ya Saba leo tarehe 10 Aprili, 2026 kwa lengo la kupitia na kujadili Rasimu ya Bajeti ya Taasisi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.
Aidha Kikao hicho Muhimu kimewakutanisha Wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimentiya WRBWB, ambapo wamepata fursa ya kuchambua kwa kina vipaumbele vya bajeti vinavyolenga kuboresha Usimamizi wa Rasilimali za Maji katika WRBWB.
Miongoni mwa maeneo yaliyopewa uzito ni pamoja na Uhifadhi wa Vyanzo vya Maji, kuimarisha Miundombinu ya Maji, pamoja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi Ndugu. Nickson Lutenda amesisitiza umuhimu wa kupanga bajeti inayozingatia mahitaji halisi ya sasa na ya baadaye hususan katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabianchi na ongezeko la mahitaji ya maji kwa matumizi ya binadamu na kiuchumi.
Katika hatua nyingine Wajumbe wamejadili mikakati ya kuongeza mapato ya Taasisi pamoja na kuboresha ushirikiano na wadau mbalimbali ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakuwa na tija na endelevu.
Kwa ujumla kikao hicho kimeweka msingi imara wa maandalizi ya Bajeti itakayowezesha WRBWB kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kulinda na kusimamia Rasilimali za Maji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
"Tonelamajilazimalihifadhiwe"




