WAMI/RUVU YASHIRIKI MAADHIMISHO YA MEI MOSI GAIRO - MOROGORO.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imeshiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro Leo tarehe 01 Mei 2026.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adamu Malima, Katika hotuba yake amewataka watumishi wa umma na sekta binafsi kuendelea kudumisha mahusiano mazuri, mshikamano na ushirikiano mahali pa kazi ili kuongeza tija na ufanisi.
Aidha Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwemo kuongeza mishahara kwa kuzingatia ufanisi wa kazi wa mtumishi mmoja mmoja.
Pia amesisitiza umuhimu wa wafanyakazi kuzingatia haki na wajibu wao pamoja na juhudi za Serikali katika kuboresha mikataba ya ajira.
Maadhimisho ya Mei Mosi huadhimishwa kila mwaka Duniani kote kama sehemu ya kutambua mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.




