WAMI/RUVU YASHIRIKI ZIARA YA WAZIRI MKUU KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI.

Bodi imeshiriki ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba iliyofanyika katika Wilaya ya Mvomero, Gairo na Kibaigwa.
Ziara hiyo ilikuwa na Lengo la Kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi pamoja na kutoa maelekezo kwa Viongozi na Taasisi husika kuhakikisha Kero hizo zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
Aidha Dkt. Mwigulu amekagu hali ya daraja la Magole lililopo eneo la Dumila na kuagiza Wananchi waruhusiwe kusafisha mto kwa kutoa mchanga katika eneo la daraja ikiwa ni Sambamba na Taasisi zote zinazohusika kukaa pamoja na kupanga utaratibu mzuri utakaotumika kuhakikisha utoaji huo wa mchanga hauathiri daraja na kingo za mto.




