Wami/Ruvu washiriki mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa kwa kutumia mfumo wa KoboToolbox.

Wami/Ruvu kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro MORUWASA wameshiriki mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa (Data Collection) kwa kutumia mfumo wa KoboToolbox yaliyotolewa na mtaalamu kutoka World Waternet leo tarehe 25 Mei 2026.
Mafunzo hayo yamelenga kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, uhifadhi na usimamizi wa taarifa kwa njia ya kidijitali huku yakitoa uelewa wa matumizi sahihi ya mfumo wa Kobo katika shughuli mbalimbali za taasisi.
Aidha mafunzo hayo yanatarajiwa kuendelea kesho kwa hatua zaidi za vitendo na matumizi ya mfumo huo katika mazingira halisi ya kazi.



