DIRA 2050
emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Katika kuidhimidha Wiki ya Mazingira Duniani, Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya mtaa Kimere, wadau wa Mazingira, kampuni na vikundi vya usafishaji wa mito wamepanda miti 500 rafiki kwa mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo mjakaranda, michikichi na miembe katika hifadhi ya Mto Mpiji, Kitongoji cha Kimere, Kata ya Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo
Lengo la zoezi hili ni kuimarisha uhifadhi wa vyanzo vya maji, kudhibiti mmomonyoko wa ardhi, kuongeza uoto wa asili na kuchangia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Mgeni Rasmi wa zoezi hili ni Bi. Stella Msofe, Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo.
Akizungumza katika zoezi hilo, Msofe amesema miti iliyopandwa inapaswa kutunzwa kwa umakini ili iweze kutoa manufaa yaliyokusudiwa kwa jamii na mazingira kwa ujumla. Pia amesema wananchi wanapaswa kuheshimu mipaka ya maeneo ya hifadhi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu zinazoweza kusababisha uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.
Aidha, amewahimiza wakazi wa Bagamoyo kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira na kudumisha usafi wa maeneo yao, akieleza kuwa wilaya hiyo ni lango muhimu la biashara, uwekezaji na utalii ambalo linahitaji mazingira safi na salama.
Kwa upande wake, Mkuu wa Ofisi ya Wami/Ruvu Dar es Salaam kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Diana Kimpute, amesema upandaji wa miti katika eneo la Kimere unalenga kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji vya Mto Mpiji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Vilevile ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka ukingo wa mto kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya uhifadhi wa mazingira na rasilimali maji.
Katika hafla hiyo, alama maalum za mipaka kati ya hifadhi ya Mto Mpiji na maeneo ya makazi ya wananchi pia zimezinduliwa ili kuimarisha ulinzi wa eneo hilo la hifadhi.
 
Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo, “Dira 2050: Tuwajibike Kukijani Tanzania.”

Mpangilio

slot gacor