WAMI/RUVU YATOA ELIMU YA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI KATIKA KATA YA LUKOBE.

WRBWB imefanya mkutano na wananchi wanaojihusishi na shughuli za kilimo kandokando ya Mto Ngerengere katika Mtaa wa Tuelewane Kata ya Lukobe,Halmashauri ya manispaa ya Morogoro.
Mkutano huu umefanyika katika eneo la Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Tuelewane chini ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo ikiwa ni baada ya kubainika kwa uvamizi katika baadhi ya maeneo ya vyanzo vya maji ambapo baadhi ya wakulima wameanza kuandaa mashamba.
Pamoja na kuwaelimisha wanachi juu ya madhara ya kilimo kisichofuata taratibu za uhifadhi wa vyanzo vya maji,wananchi pia walipatiwa mkakati wa kushirikiana na Bonde la Wam/Ruvu ili kuwa na kilimo hifadhi chenye manufaa katika kuhifadhi vyanzo vya maji na kwenye kuboresha maisha yao kama vile upandaji wa Miti ya Matunda,Minazi na Michikichi.
#ToneLaMajiLazimaLihifadhiwe



