WAMI/RUVU YATOA ELIMU KWA WASAFISHA MITO MOROGORO KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO.

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu leo Septemba 14, 2026, imefanya kikao kazi na wasafisha mito katika eneo la Lugala Manispaa ya Morogoro kwa lengo la kutoa elimu na kuwakumbusha kuhusu sheria na taratibu za usimamizi na uhifadhi wa mito na makorongo.
Aidha wadau wamepewa maelekezo ya kuendelea kusafisha mito na makorongo kwa ufanisi pamoja na kupanda miti na mimea ya asili ikiwemo matete katika kingo za mito kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji.
Katika hatua nyingine wataalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Wami)Ruvu wametoa elimu kuhusu tahadhari dhidi ya uwezekano wa mvua kubwa za El Niño huku wakitoa wito kwa wadau kuondoa vihatarishi na vitu vinavyoweza kuzuia mtiririko wa maji katika mikondo yake ya asili.
Tonelamajilazimalihifadhiwe



