emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji
Bodi ya Maji Bonde la Wami/RUVU
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC) pamoja na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NiRC) imepokea ujumbe wa tathmini kutoka Benki ya Dunia (World Bank) uliolenga kukagua utekelezaji wa Mradi wa Kimkakati wa Kuhimili Mafuriko (Flood Resilience Project).
Mradi huo unalenga kujenga mabwawa sita (6) pamoja na kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema kwa ajili ya kudhibiti mafuriko na kulinda ushoroba wa reli pamoja na wakazi wa Wilaya za Kilosa na Mpwapwa katika mabonde ya Kinyasungwe na Wami.
Katika kikao cha pamoja cha ufuatiliaji kilichofanyika katika ofisi kuu za Wami/Ruvu mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na wadau kutoka TRC, NiRC, Wizara ya Maji (MoW) pamoja na Wizara ya Ujenzi wataalamu wamewasilisha mifumo ya kisasa ya kidijitali ya utabiri wa mafuriko pamoja na juhudi mbalimbali za uhifadhi wa mazingira zinazotekelezwa chini ya mradi huo.
Aidha imeelezwa kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika kulinda miundombinu ya reli inayochangia kukuza uchumi wa taifa sambamba na kuboresha usalama wa maisha ya wananchi wanaoishi katika ushoroba wa reli.
Katika hatua nyingine Bodi imebainisha kuwa watumishi wawili wa taasisi hiyo wamerejea kutoka Korea Kusini walipokwenda kupata mafunzo ya usimamizi wa mabwawa pamoja na usimamizi wa Rasilimali za Maji kwa kutumia Teknolojia ya Akili Mnemba (AI), hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi ya maji na udhibiti wa mafuriko nchini.
"Tonelamajilazimalihifadhiwe"

Mpangilio

slot gacor